Don't miss

About Us


About Us


Sheria kwa Kiswahili inajumuisha Wataalamu wa sheria mbalimbali ambao hasa wamejikita katika kufikisha uelewa wa Sheria kwa wananchi wa kawaida kabisa na wale wanaoanza kujifunza sheria (wanafunzi). Tunasambaza vitabu mbalimbali vya sheria miongoni mwao kikiwa ni kile kitabu cha SHERIA KWA KISWAHILI vol. 1 kinachoongelea sheria za Mirathi,wosia,ndoa, watoto na baadhi ya jinai.

Hivi karibuni tutasambaza kitabu kipya cha SHERIA KWA KISWAHILI Vol.2 kitakachoongelea masuala ya ICC (the Hague) lakini yamadadavuliwa kwa Kiswahili rahisi ili kila msomaji aelewe. Kitabu hiki kimeandikwa kwa kiswahili na kinafafanua na kutoa mwongozo vizuri sana kwa viongozi wetu wa dini, viongozi wa serikali, vyama vya siasa n.k namna gani wanaweza kujikuta wamefikisha ICC kutokana na yale wanayofanya. Lengo kuu la kitabu hiki ni kuwapa onyo na kutaka Watanzania tujifunze mifano ya nchi za wenzetu waliofanya makosa, ili tuepuke migawanyiko, chuki na kuifanya Tanzania yetu iendelee kuwa nchi ya amani, umoja na mshikamano bila kujali dini, vyama vya siasa au kabila. Mungu ibariki Tanzania.

0 comments: